Acts 4:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiwe uliyemfanya mtumishi wako, baba yetu Daudi, aseme kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: ‘Kwa nini mataifa yameghadhibika? Mbona watu wamefanya mipango ya bure?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wewe ulinena kwa Roho wa Mungu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema: “ ‘Mbona mataifa wanaghadhibika, na makabila ya watu kuwaza ubatili?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba yetu Daudi alikuwa mtumishi wako. Kwa msaada wa Roho Mtakatifu aliandika maneno haya: ‘Kwa nini mataifa yanatenda kwa kiburi? Kwa nini watu wanapanga mipango isiyofaa kama hii?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndiwe uliyemfanya mtumishi wako, babu yetu Daudi, aseme kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: Kwa nini mataifa yameghadhibika? Mbona watu wamefanya mipango ya bure?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiwe uliyemfanya mtumishi wako, baba yetu Daudi, aseme kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: ‘Kwa nini mataifa yameghadhibika? Mbona watu wamefanya mipango ya bure?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wewe ulisema kwa Roho Mtakatifu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema: “ ‘Mbona watu Mataifa wanaghadhibika, na kabila za watu zinawaza ubatili?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wewe ulisema kwa Roho wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, ukasema: “ ‘Mbona mataifa wanaghadhibika, na kabila za watu zinawaza ubatili?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiwe uliyemfanya mtumishi wako, baba yetu Daudi, aseme kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: ‘Kwa nini mataifa yameghadhibika? Mbona watu wamefanya mipango ya bure?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uliisemesha Roho takatifu kwa kinywa cha mtoto wako Dawidi: Mbona wamizimu hupiga makelele?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni wewe uliyesema maneno haya kwa njia ya Roho Mutakatifu kwa kinywa cha mutumishi wako babu yetu mukubwa Daudi: ‘Kwa nini mataifa wanafanya fujo, na kwa nini watu wanafanya mipango ya ovyo?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
nawe ulinena kwa kinywa cha Daud mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na watu wametafakari ubatili?