Acts 4:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, Pontio Pilato, watu wa Israeli na watu wa mataifa walivyokutanika papa hapa mjini, kumpinga Yesu Mtumishi wako Mtakatifu ambaye ulimweka wakfu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni kweli Herode na Pontio Pilato, pamoja na watu wa Mataifa na Waisraeli, walikusanyika katika mji huu kupanga njama dhidi ya mwanao mtakatifu Isa, uliyempaka mafuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndicho hasa kilichotokea wakati Herode, Pontio Pilato, mataifa mengine na watu wa Israeli walipokusanyika pamoja hapa Yerusalemu wakawa kinyume na Yesu; Masihi, Mtumishi wako mtakatifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, Pontio Pilato, watu wa Israeli na watu wa mataifa walivyokutanika papa hapa mjini, kumpinga Yesu Mtumishi wako Mtakatifu ambaye umemtia mafuta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, Pontio Pilato, watu wa Israeli na watu wa mataifa walivyokutanika papa hapa mjini, kumpinga Yesu Mtumishi wako Mtakatifu ambaye ulimweka wakfu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu Mataifa na Waisraeli, walikusanyika katika mji huu dhidi ya mwanao mtakatifu Yesu uliyemtia mafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu wa Mataifa na Waisraeli, walikusanyika katika mji huu dhidi ya mwanao mtakatifu Isa uliyemtia mafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Maana, kwa hakika, ndivyo Herode, Pontio Pilato, watu wa Israeli na watu wa mataifa walivyokutanika papa hapa mjini, kumpinga Yesu Mtumishi wako Mtakatifu ambaye ulimweka wakfu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hii ni kweli, kwani walikusanyika mjini humu, wamkamate mtoto wako mtakatifu Yesu, uliyempaka mafuta; akina Herode na Pontio Pilato walipatana na wamizimu na watu wa Isiraeli,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ndiyo, ni kweli mufalme Herode, naye mutawala Pontio Pilato walikusanyika katika muji huu pamoja na Waisraeli na watu wa mataifa mengine kwa kufanya shauri baya juu ya mutumishi wako mutakatifu Yesu, uliyemuchagua kuwa Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,