Acts 4:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyosha mkono wako ili uponye watu. Fanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu Mtumishi wako Mtakatifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyoosha mkono wako ili kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miujiza kwa jina la Mwanao mtakatifu Isa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tusaidie, ili tuwe jasiri kwa kutuonesha nguvu zako. Ponya Wagonjwa. Fanya ishara na maajabu kutokea kwa mamlaka ya Yesu mtumishi wako mtakatifu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nyosha mkono wako uponye watu. Fanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu Mtumishi wako Mtakatifu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyosha mkono wako ili uponye watu. Fanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu Mtumishi wako Mtakatifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyosha mkono wako ili kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miujiza kwa jina la Mwanao mtakatifu Yesu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyoosha mkono wako ili kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miujiza kwa jina la Mwanao mtakatifu Isa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyosha mkono wako ili uponye watu. Fanya ishara na maajabu kwa jina la Yesu Mtumishi wako Mtakatifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unyoshe mkono, uponye watu na kufanya vielekezo na vioja kwa Jina la mtoto wako mtakatifu Yesu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utumie nguvu zako kwa kuponyesha watu, kwa kufanya maajabu na vitambulisho kwa uwezo wa jina la mutumishi wako mutakatifu Yesu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.