Acts 5:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mitume walifanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Waumini wote walikuwa wakikusanyika katika Ukumbi wa Sulemani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mitume walipewa nguvu ya kufanya ishara nyingi za miujiza na maajabu katikati ya watu. Walikuwa wanakutanika pamoja mara kwa mara katika eneo la Hekalu lililoitwa Ukumbi wa Sulemani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Nao wale wote walioamini walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Solomoni kwa nia moja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Walioamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Sulemani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mitume walifanya miujiza na maajabu mengi kati ya watu. Waumini walikuwa wakikutana pamoja katika ukumbi wa Solomoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vikafanyika vielekezo na vioja vingi kwa mikono ya mitume kwa watu wa kwao, wale wote wakiwa pamoja katika ukumbi wa Salomo, kwa sababu mioyo yao ilikuwa ilikuwa mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mitume walifanya maajabu na vitambulisho vingi katikati ya watu. Waamini wote walizoea kukusanyika katika Baraza wanaloliita La Solomono.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu: nao wote walikuwa kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani: