Acts 5:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kandokando ya Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu, nao wote wakaponywa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu walikuja kutoka katika miji kuzunguka Yerusalemu. Waliwaleta wagonjwa au waliosumbuliwa na pepo wachafu. Wote waliponywa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kando kando ya Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu, nao wote wakaponywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kandokando ya Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu, nao wote wakaponywa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia watu wakakusanyika kutoka katika miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu, hao wote wakaponywa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo makundi ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengi walifika kutoka katika miji ya kandokando ya Yerusalemu, wakiwaleta wagonjwa wao na wale waliokuwa na pepo wachafu, nao wote wakaponywa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakakusanyika hata watu wengi wa vijiji vilivyouzunguka Yerusalemu, wakaleta wagonjwa nao wenye kupagawa na pepo wachafu, wakaponywa wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo makutano ya watu wa miji iliyoko kandokando ya Yerusalemu wakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu; nao wote wakaponywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wengi vilevile kutoka miji inayokuwa pembeni ya Yerusalema walikusanyika, wakiwaleta wagonjwa na watu wanaoteswa na pepo, na wote wakaponyeshwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nayo makutano ya miji ilioyo kando kando ya Yerusalemi yakakutanika, wakileta wagonjwa, nao walioudhiwa na pepo wachafu: nao wote wakaponywa.