Acts 5:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
lakini aliwapa mitume sehemu tu ya pesa alizopata baada ya kuuza shamba lake. Kwa siri alibakiza kiasi cha pesa kwa ajili yake mwenyewe. Mke wake alilijua hili na akalikubali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akihifadhi kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, mkewe akiwa anajua, Anania akajiwekea sehemu ya fedha alizopata na ile sehemu nyingine akawakabidhi mitume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akaficha fungu la fedha, alizozipata, naye mkewe alivijua. Kisha akaleta fungu moja, akaliweka miguuni pa mitume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini akaficha sehemu ya feza alizopata na kuleta sehemu iliyobaki kwa mikono ya mitume. Muke wake alijua maneno hayo yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe nae akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.