Acts 5:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mitume walitii, wakaingia hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu na halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi, halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya Baraza la Wayahudi, yaani wazee wote wa Israeli. Wakatumana wale mitume waletwe kutoka gerezani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mitume waliposikia hili, walifanya kama walivyoambiwa. Walikwenda katika eneo la Hekalu asubuhi na mapema jua lilipokuwa linachomoza na kuanza kuwafundisha watu. Kuhani mkuu na wafuasi wake wakakusanyika na kuitisha mkutano wa Baraza kuu na wazee wa Kiyahudi. Wakawatuma baadhi ya watu gerezani ili wawalete mitume kwao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mitume walitii, wakaingia Hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani Mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu, yaani halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mitume walitii, wakaingia hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu na halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi, halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani Mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mitume walitii, wakaingia hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu na halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi, halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipoyasikia haya wakapaingia Patakatifu, kulipokucha, wakafundisha. Lakini mtambikaji mkuu nao waliokuwa pamoja naye wakaja, wakawakusanya wenzao wakuu na wazee wote wa wana wa Isiraeli, wakatuma watu bomani, wawalete.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sawa vile walivyoambiwa, asubui mapema wakaingia ndani ya hekalu, na kuanza kuwafundisha watu. Kuhani Mukubwa na wale washiriki walipofika, wakawakusanya wasimamizi wote wa Waisraeli kwa kufanya mukutano wa Baraza Kubwa. Nao wakawatuma watu kwenye kifungo kwa kuwaleta mitume.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete.