Acts 5:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkuu wa walinzi wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani walipolisikia hili, walichanganyikiwa na kujiuliza maana yake ni nini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mkuu wa walinzi wa Hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkuu wa walinzi wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu, viongozi na makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mlinzi mkuu wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkuu wa walinzi wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia habari hiyo wakawa na wasiwasi, wasijue yaliyowapata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mlinda Patakafitu nao watambikaji wakuu walipoyasikia maneno haya wakahangaika sana, wasijue, jambo hilo litakavyokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukubwa wa walinzi wa hekalu na wakubwa wa makuhani waliposikia habari hii, wakakuwa na wasiwasi sana, wakijiuliza ni nini itakayotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kuhani mkuu na jemadari wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia haya, wakaingiwa na mashaka kwa ajili yao, yatakuwaje mambo hayo.