Acts 5:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho wa Mungu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akasema, “Anania, kwa nini umemruhusu Shetani aitawale akili yako kwa wazo la namna hii? Umebakiza sehemu ya pesa kwa ajili yako mwenyewe na kumdanganya Roho Mtakatifu!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho wa Mwenyezi Mungu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuhifadhi kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Petro akamwuliza, “Anania, mbona Shetani ameuingia moyo wako na kukufanya umdanganye Roho Mtakatifu kwa kujiwekea sehemu ya fedha ulizopata kutokana na lile shamba?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Petero akasema: Anania, mbona Satani ameenea moyoni mwako, ukamdanganya Roho Mtakatifu na kuficha fungu la fedha za kiunga?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Petro akamwuliza: “Anania, namna gani Shetani amekuingia hata akakusemesha uongo mbele ya Roho Mutakatifu na kuficha sehemu ya feza ulizopata ulipouzisha lile shamba?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja?