Acts 5:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu 400 wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao mia nne walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnakumbuka Theuda alipotokea? Alijidai kuwa alikuwa mtu mkuu, na wanaume kama mia nne waliungana naye. Lakini aliuawa na wote waliomfuata walitawanyika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu mia nne wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu 400 wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana wakati uliopita aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda ambaye alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao 400 walioambatana naye. Lakini aliuawa na wafuasi wake wote wakatawanyika na kupotea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao 400 walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapatao mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zamani kidogo, kulitokea mtu mmoja jina lake Theuda, akajisema kuwa mtu wa maana na watu karibu 400 wakajiunga naye. Lakini aliuawa, kisha wafuasi wake wote wakatawanyika na kikundi chake kikafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mbele ya siku hizi aliondokea Teuda, akajiwazia, kwamba yeye ndiye mtu, nao watu waliomfuata wakapata kama 400. Alipouawa, wote waliomtii wakatawanyika, wakapoteapotea, tena hakuna kitu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Haijapita siku nyingi kulitokea mutu mumoja aliyeitwa Teuda. Akajidai kuwa mutu mukubwa, na karibu watu mia ine walijiunga naye. Lakini akauawa na wanafunzi wake wote wakasambazwa na kutosemekana tena.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akidai ya kuwa yeye ni mtu, mkuu watu wapata aroba mia wakashikamana nae, na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.