Acts 5:37 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya. Huyu naye aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa, na wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadaye, wakati wa sensa, mtu mmoja aitwaye Yuda alikuja kutoka Galilaya. Watu wengi walijiunga kwenye kundi lake, lakini yeye pia aliuawa na wafuasi wake wote walitawanyika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya. Huyu naye, aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa, na wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya. Huyu naye aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa, na wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada yake alitokea Yuda Mgalilaya wakati ule wa kuandikwa orodha ya watu akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye naye aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadhaa nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, baadaye, wakati ule wa kuhesabiwa watu, alitokea Yuda wa Galilaya. Huyu naye aliwavuta watu wakamfuata; lakini naye pia aliuawa, na wafuasi wake wakatawanyika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha katika siku za kuandikiwa kodi aliondokea Yuda Mgalilea, akatenga kikundi cha watu, wamfuate yeye. Naye alipoangamia, wote waliomtii wakatawanyika nao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma yake, katika siku zile walipofanya hesabu ya watu, kulitokea Yuda wa jimbo la Galilaya. Huyo naye aliwavuta watu wengine kwa kumufuata. Lakini yeye vilevile aliuawa na wanafunzi wake wote wakasambazwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa kodi, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma yake, nae akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika.