Acts 6:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manunguniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinungunika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, Wayahudi wa Kiyunani walinung’unika dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawo wa chakula wa kila siku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wengi zaidi walipokuwa wafuasi wa Yesu. Wafuasi waliokuwa wakizungumza Kiyunani walianza kuwalalamikia wafuasi wenzao waliokuwa wanazungumza Kiebrania au Kiaramu. Walisema kuwa wajane wao walikuwa hawapewi mgao wao kutokana na kile wafuasi walikuwa wanapewa kila siku.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manung'uniko kati ya wanafunzi waliosema Kigiriki na wale waliosema Kiebrania. Wale waliosema Kigiriki walinung'unika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manung'uniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinung'unika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manung'uniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manung’uniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kigiriki juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manunguniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinungunika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile wanafunzi walipozidi kuwa wengi, Wagriki waliwanung'unikia Waebureo, kwani wanawake wajane wa kwao hawakutumikiwa kama wengine na kugawiwa kila siku vilivyowapasa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung’uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile, kufuatana na jinsi hesabu ya wanafunzi wa Yesu ilivyokuwa ikizidi kuongezeka, kulitokea manunguniko kati ya Wayuda waliosema Kigriki na Wayuda waliosema Kiebrania. Wale waliosema Kigriki walinungunika kwa sababu wajane wao walisahauliwa wakati wa kugawanya vifaa vya kila siku.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.