Acts 6:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”, nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa) la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na jimbo la Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini baadhi ya Wayahudi pale waliotoka katika sinagogi la Watu Huru, kama lilivyoitwa. Kundi hili lilijumuisha Wayahudi kutoka Kirene, Iskanderia, Kilikia na Asia. Walianza kubishana na Stefano.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”, nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”, nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa), la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, ukainuka upinzani wa watu wa Sinagogi la Watu Huru (kama lilivyokuwa linaitwa), la Wayahudi wa Kirene na wa Iskanderia, na wengine kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa wakaanza kupingana na Stefano.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu fulani wakatokea ili wabishane na Stefano. Baadhi ya watu hao walikuwa wa sunagogi moja lililoitwa “Sunagogi la Watu Huru”, nao walitoka Kurene na Aleksandria; wengine walitoka Kilikia na Asia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo wakainuka wengine waliokuwa wa chama kilichoitwa cha Walibertino na watu wa Kirene na wa Alekisandria nao walitoka Kilikia na Asia, wakaulizana na Stefano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kukatokea watu wamoja waliopingana na Stefano. Watu hawa walikuwa wa nyumba ya kuabudia iliyojulikana kwa jina la “Wenye Uhuru.” Nao walitoka katika inchi ya Kurene na ya Alesanduria, na kutoka jimbo la Kilikia na la Azia. Watu hawa wakaanza kubishana na Stefano
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano: