Acts 7:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akamwokoa katika taabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hata Farao akamweka awe mkuu wa ile nchi na nyumba ya kifalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwokoa kutoka mateso yote yaliyompata. Tena Mungu akampa Yusufu kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Naye Farao akamweka kuwa mtawala wa Misri na wa jumba lote la kifalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
akamwokoa kutoka katika matatizo yake yote. Wakati huo Farao alikuwa mfalme wa Misri. Alimpenda na akamheshimu Yusufu kwa sababu ya hekima ambayo Mungu alimpa. Farao alimfanya Yusufu kuwa gavana wa Misri na msimamizi wa watu wote na kila kitu katika kasri lake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akamwokoa katika taabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hata Farao akamweka awe mkuu wa ile nchi na nyumba ya kifalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akamwokoa katika taabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hata Farao akamweka awe mkuu wa ile nchi na nyumba ya kifalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwokoa kutoka katika mateso yote yaliyompata, tena akampa kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimweka kuwa mtawala juu ya Misri na juu ya jumba lote la kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwokoa kutoka mateso yote yaliyompata, tena akampa kibali na hekima aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri, ambaye alimweka kuwa mtawala juu ya Misri na juu ya jumba lote la kifalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akamwokoa katika taabu zake zote. Mungu alimjalia fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri, hata Farao akamweka awe mkuu wa ile nchi na nyumba ya kifalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamwokoa katika maumivu yake yote, akamgawia kipaji cha werevu wa kweli, apate kusema mbele ya Farao, mfalme wa Misri; ndiye aliyemweka kuwa mkubwa, aitawale Misri na nyumba yake yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akamwokoa toka katika taabu yote aliyopata. Mungu akamujalia neema, apate kupendwa na Mufalme wa Misri na kuonekana kuwa mwenye hekima mbele yake. Mufalme yule akamuweka kuwa musimamizi wa inchi yake na wa nyumba yake yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akamtoa katika misiba yake yote, akampa kibali na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri: nae akamfanya msimamizi wa Misri na nyumba yake yote.