Acts 7:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika safari yao ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, na Farao akaifahamu jamaa ya Yosefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipoenda mara ya pili, Yusufu alijitambulisha kwa ndugu zake; naye Farao akapata habari kuhusu ndugu za Yusufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata safari ya pili Yusufu akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusufu ikawa dhahiri kwa Farao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha walikwenda safari ya pili. Safari hii Yusufu akawaeleza ndugu zake yeye ni nani. Ndipo Farao akatambua kuhusu familia ya Yusufu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Katika safari yao ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, na Farao akaifahamu jamaa ya Yosefu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika safari yao ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, na Farao akaifahamu jamaa ya Yosefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokwenda mara ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, nao ndugu zake Yosefu wakajulishwa kwa Farao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokwenda mara ya pili, Yusufu alijitambulisha kwa ndugu zake, nao ndugu zake Yusufu wakajulishwa kwa Farao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata safari ya pili Yusufu akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusufu ikawa dhahiri kwa Farao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika safari yao ya pili, Yosefu alijitambulisha kwa ndugu zake, na Farao akaifahamu jamaa ya Yosefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika safari ya pili Yosefu akajitambilisha kwa ndugu zake, nako kwa Farao ukoo wa Yosefu ukajulika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata safari ya pili Yusufu akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusufu ikawa dhahiri kwa Farao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa safari ya pili, Yosefu akajitambulisha kwa wandugu zake, naye Mufalme wa Misri akapata kujua jamaa ya Yosefu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta safari ya pili Yusuf akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusuf ikawa dhahiri kwa Farao.