Acts 7:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miili yao ililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alikuwa amenunua kutoka kwa kabila la Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Ibrahimu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadaye, miili yao ilihamishiwa Shekemu, ambako iliwekwa katika kaburi ambalo Ibrahimu alilinunua kwa fedha kutoka kwa wana wa Hamori.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Miili yao ililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katika kaburi Abrahamu alilonunua kutoka kwa kabila la Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miili yao ililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alikuwa amenunua kutoka kwa kabila la Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Ibrahimu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Abrahamu alilinunua kwa kima fulani cha fedha kutoka kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miili yao ililetwa mpaka Shekemu, ikazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alikuwa amenunua kutoka kwa kabila la Hamori kwa kiasi fulani cha fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakapelekwa Sikemu, wakazikwa katika kaburi, alilolinunua Aburahamu na fedha kwa wana wa Hamori kule Sikemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maiti zao zikapelekwa katika jimbo la Sekemu na kuzikwa katika kaburi lile Abrahamu alilonunua kwa feza kutoka kwa wazao wa Hemora.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakachukuliwa hatta Sukem wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa kimo cha fedha kwa wana wa Emmor, huko Sukem.