Acts 7:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko alimwona mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na kwa kulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri. (
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliona mmoja wao ananyanyaswa na Mmisri, hivyo akamtetea; Musa akampiga na kumwua Mmisri ili kulipiza kwa kumwumiza Mwisraeli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huko alimwona mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na kulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko alimwona mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na kwa kulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri. (
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliona mmoja wao akionewa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamwua kulipiza kisasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipizia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko alimwona mmoja wao akitendewa vibaya, akaenda kumwokoa, na kwa kulipiza kisasi, akamuua yule Mmisri. (
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoona, mmoja anavyoumizwa bure tu, akamsaidia yule aliyepigwa, akamlipiza yule Mmisri akimwua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule akamwona Mumisri mumoja akimutendea mumoja wa wale wandugu zake vibaya. Basi akamusaidia yule aliyeonewa; akalipiza kisasi kwa kumwua yule Mumisri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamhami, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga Mmisri.