Acts 7:27 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema: ‘Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wetu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini yule mtu aliyekuwa akimdhulumu mwenzake akamsukuma Musa kando, akamuuliza, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliyekuwa akimwumiza mwenzake akamsukuma Musa na akamwambia, ‘Nani amekufanya wewe uwe mtawala na mwamuzi wetu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema: Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wa watu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema: ‘Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wetu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini yule mtu aliyekuwa akimwonea mwenzake akamsukuma Mose kando, akamwuliza, ‘Ni nani alikuweka uwe mtawala na mwamuzi juu yetu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini yule mtu aliyekuwa akimdhulumu mwenzake akamsukuma Musa kando, akamuuliza, ‘Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule aliyekuwa anampiga mwenzake alimsukuma Mose kando akisema: ‘Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi wetu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yule aliyemkorofisha mwenziwe akamsukuma akisema: Yuko nani aliyekuweka kuwa mkuu mwamuzi kwetu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yule aliyekuwa akimutendea mwenzake vibaya akamusukuma Musa pembeni akisema: ‘Nani aliyekuweka wewe kuwa mukubwa na mwamuzi wetu?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu wetu, na mwamuzi wetu?