Acts 7:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kusikia hayo, Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani na huko akapata watoto wawili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Musa aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Musa alipomsikia akisema hili, alikimbia Misri. Alikwenda kuishi Midiani kama mgeni. Katika kipindi alichoishi huko, alipata wana wawili.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kusikia hayo Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani na huko akapata watoto wawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kusikia hayo, Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani na huko akapata watoto wawili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mose aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Musa aliposikia maneno haya, alikimbilia huko Midiani alikokaa kama mgeni, naye akapata watoto wawili wa kiume.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa kama mgeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kusikia hayo, Mose alikimbia, akaenda kukaa katika nchi ya Midiani na huko akapata watoto wawili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya neno hilo Mose akakimbia, akawa mgeni katika nchi ya Midiani. Ndiko, alikozaa wana wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa ajili ya maneno hayo akakimbia na kwenda kukaa katika inchi ya Midiani. Na kule akazaa wana wawili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya mgeni katika inchi ya Madiani, akazaa wana wawili huko.