Acts 7:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu alimwambia: ‘Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonesha!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akamwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na katika jamii yako, uende hadi nchi nitakayokuonesha.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonyesha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alimwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na watu wako, kisha uende katika nchi nitakayokuonesha.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu alimwambia: Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonyesha!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu alimwambia: ‘Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonesha!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akamwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na kutoka kwa jamii yako uende katika nchi nitakayokuonyesha.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akamwambia, ‘Ondoka kutoka nchi yako na kutoka kwa jamii yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonesha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu alimwambia: ‘Ondoka katika nchi yako; waache watu wa ukoo wako; nenda katika nchi nitakayokuonesha!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamwambia: Toka katika nchi yako kwenye ndugu zako, uende katika nchi, nitakayokuonyesha!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonyesha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu alimwambia: ‘Toka katika inchi yako na uache wandugu zako, uende katika inchi nitakayokuonyesha.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Toka katika inchi yako na katika jamaa zako, ukaende hatta inchi nitakayokuonyesha.