Acts 7:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiye aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabu katika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani, kwa muda wa miaka arubaini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliwaongoza Waisraeli kutoka Misri baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo Musa aliwaongoza watu kutoka Misri. Alitenda maajabu na ishara za miujiza Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani kwa miaka arobaini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndiye aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabu katika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani kwa muda wa miaka arobaini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiye aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabu katika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani, kwa muda wa miaka arubaini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliwaongoza wana wa Israeli kutoka Misri, baada ya kufanya ishara na maajabu mengi huko Misri, katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa muda wa miaka arobaini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiye aliyewaongoza wale watu watoke Misri kwa kufanya miujiza na maajabu katika nchi ya Misri, katika bahari ya Shamu na jangwani, kwa muda wa miaka arubaini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha huyo akawatoa na kufanya vioja na vielekezo katika nchi ya Misri na katika Bahari Nyekundu, kisha nako jangwani miaka 40.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye ndiye aliyewaongoza Waisraeli toka Misri akifanya maajabu na vitambulisho katika inchi ile, na kwenye bahari Nyekundu na katika jangwa kwa muda wa miaka makumi ine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika inchi ya Misri, na katika bahari ya Sham, na katika jangwa muda wa miaka arubaini.