Acts 7:38 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waisraeli walipokusanyika kule jangwani, Mose ndiye aliyekuwako huko kama mjumbe kati ya hao wazee wetu na yule malaika aliyeongea naye mlimani Sinai. Ndiye aliyekabidhiwa yale maneno ya uhai atupe sisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu ndiye yule Musa aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Musa huyo huyo alikuwa pamoja na kusanyiko la watu wa Mungu jangwani. Alikuwa na malaika aliyezungumza naye alipokuwa Mlima Sinai, na alikuwa pamoja na baba zetu. Alipokea maneno yaletayo uzima kutoka kwa Mungu, na Musa akatupa sisi Maneno hayo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati watu wa Israeli walipokutana pamoja kule jangwani, Mose ndiye aliyekuwako huko pamoja nao. Alikuwa huko pamoja na babu zetu na yule malaika aliyeongea naye mlimani Sinai; ndiye aliyekabidhiwa yale maneno yaletayo uzima atupe sisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waisraeli walipokusanyika kule jangwani, Mose ndiye aliyekuwako huko kama mjumbe kati ya hao wazee wetu na yule malaika aliyeongea naye mlimani Sinai. Ndiye aliyekabidhiwa yale maneno ya uhai atupe sisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu ndiye yule Mose aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu ndiye yule Musa aliyekuwa katika kusanyiko huko jangwani, ambaye malaika alisema naye pamoja na baba zetu kwenye Mlima Sinai, naye akapokea maneno yaliyo hai ili atupatie.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima ili atupe sisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waisraeli walipokusanyika kule jangwani, Mose ndiye aliyekuwako huko kama mjumbe kati ya hao wazee wetu na yule malaika aliyeongea naye mlimani Sinai. Ndiye aliyekabidhiwa yale maneno ya uhai atupe sisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
huyo ndiye aliyekuwa penye wateule jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye mlimani kwa Sinai, tena pamoja na baba zetu. Ndiye aliyepokea maneno ya uzima, atupe sisi;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na wakati ule kulipokuwa mukutano wa Waisraeli katika jangwa, yeye alikuwa pale pamoja na babu zetu na yule malaika aliyesema naye kwenye mulima Sinai. Na ni yeye aliyefunuliwa ujumbe wa Mungu unaoleta uzima na kuutangaza kwetu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.