Acts 7:41 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo ndipo walipojitengenezea sanamu ya ndama, wakaitambikia na kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi ya mikono yao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo watu wakatengeneza kinyago kinachofanana na ndama. Kisha wakakitolea sadaka za kuteketezwa. Walifurahia kile walichotengeneza kwa mikono yao wenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo ndipo walipojitengenezea sanamu ya ndama, wakaitambikia na kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi ya mikono yao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo ndipo walipojitengenezea sanamu ya ndama, wakaitambikia na kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi ya mikono yao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huu ndio wakati walipotengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichotengeneza kwa mikono yao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huu ni ule wakati walitengeneza sanamu katika umbo la ndama, wakailetea sadaka kufanya maadhimisho kwa ajili ya kile kitu walichokitengeneza kwa mikono yao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatengeneza ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo ndipo walipojitengenezea sanamu ya ndama, wakaitambikia na kukifanyia sherehe kitu ambacho ni kazi ya mikono yao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile wakatengeneza ndama, nacho kinyago hicho wakakitolea ng'ombe za tambiko, nacho kilichokuwa kazi ya mikono yao wakakishangilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile wakajitengenezea sanamu ya mwana-ngombe, wakaitambikia na kufurahia kitu hicho walichojifanyia wao wenyewe.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi ya mikono yao.