Acts 7:42 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: ‘Enyi watu wa Israeli! Si mimi mliyenitolea tambiko na sadaka kwa miaka arubaini kule jangwani!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mungu akageuka, akawaachia waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii: “ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka kwa miaka arobaini kule jangwani, ee nyumba ya Israeli?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Mungu akawaacha, nao wakaendelea kuabudu nyota na sayari. Kitabu cha manabii kinasema hivi: ‘Watu wa Israeli, hamkunipa dhabihu jangwani kwa miaka arobaini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: Enyi watu wa Israeli! Si mimi mliyenitolea dhabihu na sadaka kwa muda wa miaka arobaini kule jangwani!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: ‘Enyi watu wa Israeli! Si mimi mliyenitolea tambiko na sadaka kwa miaka arubaini kule jangwani!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Mungu akageuka, akawaacha waabudu jeshi lote la mbinguni kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: “ ‘Je, mlinitolea Mimi dhabihu na sadaka kwa kipindi cha miaka arobaini kule jangwani, enyi nyumba ya Israeli?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Mungu akageuka, akawaacha waabudu jeshi lote la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Manabii: “ ‘Je, mliniletea dhabihu na sadaka kwa miaka arobaini kule jangwani, ee nyumba ya Israeli?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Mungu aliondoka kati yao, akawaacha waabudu nyota za anga, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii: ‘Enyi watu wa Israeli! Si mimi mliyenitolea tambiko na sadaka kwa miaka arubaini kule jangwani!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Mungu akageuka, akawatupa, wavitumikie vikosi vya mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Wafumbuaji: Je? Ng'ombe na vipaji, mlivyovitoa nyikani miaka 40, vilikuwa vya kunitambikia mimi, ninyi mlio mlango wa Isiraeli?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Mungu akajitenga mbali nao, akawaacha waabudu nyota, jua na mwezi kufuatana na maneno haya yaliyoandikwa katika kitabu cha manabii: ‘Ninyi watu wa Israeli, si mimi muliyemuchinjia nyama na kumutolea sadaka zingine kwa muda wa ile miaka makumi ine katika jangwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Mungu akaghairi, akawaacha, wakaliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, Je! mlinitolea dhabihu na sadaka Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?