Acts 7:43 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki, na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu. Kwa sababu hiyo nitawapeleka mateka mbali kupita Babuloni!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki, na nyota ya mungu wenu Refani, vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu. Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlibeba hema kwa ajili ya kumwabudia Moleki, na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Hizi zilikuwa sanamu mlizotengeneza ili mziabudu. Hivyo nitawahamishia mbali, kuvuka Babeli.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki, na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu. Kwa sababu hiyo nitakupeleka mateka mbali kupita Babuloni!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki, na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu. Kwa sababu hiyo nitawapeleka mateka mbali kupita Babuloni!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki na ya mungu wenu Refani, vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu. Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
La, ninyi mliinua madhabahu ya Moleki, na nyota ya mungu wenu Refani, vinyago mlivyotengeneza ili kuviabudu. Kwa hiyo nitawapeleka mbali’ kuliko Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi mlikibeba kibanda cha mungu Moloki, na sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Sanamu mlizozifanya ndizo mlizoabudu. Kwa sababu hiyo nitawapeleka mateka mbali kupita Babuloni!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapana, ila mlikuwa mmejitwika hema la Moloko na nyota za mungu wa Romfa; hivyo vinyago, mlivyovitengeneza, ndivyo, mlivyovitumia vya kuviangukia. Kwa hiyo nitawahamisha ninyi, mwende mbali kupita Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulitembea mukibeba hema ya mungu wenu Moleki nayo sanamu ya nyota ya mungu wenu Refani. Mulijitengenezea sanamu hizo kusudi muziabudu. Kwa hiyo nitawahamisha mbali kupita muji Babeli.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nanyi mlichukua khema ya Molok, Na nyota za mungu wenu Refan, Sanamu mlizozifanya illi kuziabudu: Nami nitawabamisha mwende mbali hatta Babel.