Acts 7:44 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema la maamuzi. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili ya kile alichooneshwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani, ambalo lilitengenezwa kama Mungu alivyomwelekeza Musa, kulingana na kielelezo alichokiona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawasawa na mfano ule aliouona;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baba zetu walikuwa na Hema Takatifu walipokuwa jangwani. Mungu alimwelekeza Musa jinsi ya kutengeneza hema hii. Aliitengeneza kwa kufuata ramani aliyoonyeshwa na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema lililoshuhudia kuweko kwa Mungu. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili ya kile alichoonyeshwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema la maamuzi. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili ya kile alichooneshwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Mose, kulingana na kielelezo alichoona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Baba zetu walikuwa na lile Hema la Ushuhuda huko jangwani. Lilikuwa limetengenezwa kama Mungu alivyokuwa amemwelekeza Musa, kulingana na kielelezo alichoona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye kulingana na mfano ule aliouona;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kule jangwani babu zetu walikuwa na lile hema la maamuzi. Lilitengenezwa kama Mungu alivyomwambia Mose alifanye; nakala kamili ya kile alichooneshwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baba zetu walipokuwa jangwani walikuwa nalo lile Hema la Ushahidi, kama mwenye kusema na Mose alivyoagiza na kumwambia, alitengeneze kwa mfano, aliouona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawasawa na mfano ule aliouona;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kule katika jangwa babu zetu walikuwa na ile hema inayokuwa na vibao vya agano ndani yake. Hema ile ilikuwa imetengenezwa kama vile Mungu alivyomwagiza Musa, na mufano ule alioonyeshwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ile khema ya shahada ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawa sawa na mfano ule aliouona;