Acts 7:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu hakumpa hata sehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hata hivyo, alimwahidi kumpa nchi hii iwe yake na ya wazawa wake, ingawaje wakati huu hakuwa na mtoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu hakumpa urithi wowote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Mungu hakumpa Ibrahimu sehemu yoyote ya ardhi hii, hata eneo dogo lenye ukubwa wa unyayo wake. Lakini Mungu aliahidi kuwa atampa Ibrahimu nchi hii yeye na watoto wake hapo baadaye. Hii ilikuwa kabla Ibrahimu hajapata watoto.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu hakumpa hata sehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hata hivyo, alimwahidia kumpa nchi hii iwe yake na ya wazawa wake, ingawaje wakati huu hakuwa na mtoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu hakumpa hata sehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hata hivyo, alimwahidi kumpa nchi hii iwe yake na ya wazawa wake, ingawaje wakati huu hakuwa na mtoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu hakumpa urithi wo wote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Abrahamu hakuwa na mtoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu hakumpa urithi wowote katika nchi hii, hakumpa hata mahali pa kuweka wayo mmoja. Bali Mungu alimwahidi kuwa yeye na uzao wake baada yake wangeirithi hii nchi, ingawa wakati huo Ibrahimu hakuwa na mtoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu hakumpa hata sehemu moja ya nchi hii iwe mali yake; hata hivyo, alimwahidi kumpa nchi hii iwe yake na ya wazawa wake, ingawaje wakati huu hakuwa na mtoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hakumpa fungu humu, ingawa liwe limelingana na wayo; ila alipokuwa hana mtoto, aliagana naye, ya kuwa atampa, aitwae nchi hii yeye nao wa uzao wake wajao nyuma yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule Mungu hakumupa Abrahamu hata sehemu ndogo ya shamba inayokuwa kama kikanyagio cha muguu kuwa urizi wake, lakini alimwahidi kwamba atamupa inchi hii kuwa urizi wake na wa wazao wake watakaoishi nyuma yake. Wakati ule, alikuwa hana mutoto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala hakumpa urithi humu hatta kiasi cha kuweka mguu: akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya, uzao wake baadae, alipokuwa hana mtoto.