Acts 7:60 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alianguka kwa magoti yake na kupaza sauti, akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii!” Haya yalikuwa maneno yake ya mwisho kabla ya kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa, akasema, “Bwana Isa, usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema hayo, akalala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona kitendo cha kuuawa kwake kuwa sawa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kubwa: “Bwana, usiwalaumu kwa sababu ya dhambi hii.” Baada ya kusema hivyo, akafa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akapiga magoti, akaita kwa sauti kuu: Bwana, usiwawekee kosa hili! Alipokwisha kuyasema haya akalala.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akapiga magoti, akalalamika, akisema: “Bwana, usiwahesabie zambi hii.” Na nyuma ya kusema maneno haya, akakufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala.