Acts 7:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu Mungu akafanya naye agano ambalo tohara ni ishara yake. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akampa Ibrahimu agano la tohara. Naye Ibrahimu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale baba zetu wa zamani kumi na wawili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akampa agano la tohara; basi Ibrahimu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu aliweka agano na Ibrahimu; alama ya agano hili ilikuwa tohara. Na Ibrahimu alipopata mwana, alimtahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa. Jina la mwanaye lilikuwa Isaka. Pia, Isaka alimtahiri mwanaye Yakobo. Na Yakobo alifanya vivyo hivyo kwa wanaye, ambao ndiyo baba wakuu kumi na mbili wa watu wetu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Halafu Mungu aliifanya tohara iwe ishara ya agano. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka, siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu Mungu akafanya naye agano ambalo tohara ni ishara yake. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akampa Abrahamu Agano la tohara. Naye Abrahamu akamzaa Isaki na kumtahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa kwake. Baadaye Isaki akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale wazee wetu wakuu kumi na wawili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akampa Ibrahimu Agano la tohara. Naye Ibrahimu akamzaa Isaka na kumtahiri siku ya nane. Baadaye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa wale wazee wetu kumi na wawili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu Mungu akafanya naye agano ambalo tohara ni ishara yake. Hivyo, Abrahamu alimtahiri mtoto wake Isaka siku ya nane baada ya kuzaliwa. Na Isaka, vivyo hivyo, alimtahiri Yakobo. Naye Yakobo aliwatendea wale mababu kumi na wawili vivyo hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akampa agano la tohara; kwa hiyo alipomzaa Isaka akamtahiri siku ya nane; naye Isaka akamzaa Yakobo, naye Yakobo akawazaa babu zetu wakuu kumi na wawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akampa agano la tohara; basi Ibrahimu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Mungu akafanya agano na Abrahamu, na kitambulisho cha kuhakikisha kwamba limeshikwa kilikuwa kutahiriwa. Kwa hiyo Abrahamu akamutahiri mwana wake Isaka alipotimiza siku nane za kuzaliwa. Naye Isaka akamutahiri mwana wake Yakobo, na Yakobo akawatahiri wana wake kumi na wawili waliokuwa babu zetu wakubwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akampa agano la Tohara; bassi Ibrahimu akazaa Isaak, akamtahiri siku ya nane. Isaak akamzaa Yakobo, Yakobo akawazaa wale thenashara, wazee wetu.