Acts 8:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri Injili ya ufalme wa Mungu na jina la Isa Al-Masihi, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Filipo alipowahubiri watu Habari Njema kuhusu Ufalme wa Mungu na Nguvu za Yesu Kristo. Wanaume na wanawake waliamini alichosema Filipo na wakabatizwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, wakabatizwa wanaume na wanawake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini watu walipomwamini Filipo alipohubiri habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu na jina la Isa Al-Masihi, wakabatizwa wanaume na wanawake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walipomtegemea Filipo aliyewapigia mbiu njema ya ufalme wa Mungu na ya Jina la Yesu Kristo, wakabatizwa, waume na wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini walipoamini Habari Njema ambayo Filipo alihubiri juu ya Ufalme wa Mungu na juu ya Yesu Kristo, wanaume na wanawake wakabatizwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini walimpomwamini Filipo, akizikhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.