Acts 8:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Simoni alingamua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho wa Mungu mitume walipoweka mikono juu yao, akataka kuwapa fedha
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Simoni aliyekuwa mchawi alipoona Roho Mtakatifu anatolewa kwa watu kwa kuweka mikono juu yao. Aliwapa pesa mitume.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo Simoni aling'amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Simoni aling'amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho Mtakatifu mitume walipoweka mikono juu yao, akawapa fedha
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Simoni alipoona kuwa watu wanapokea Roho wa Mwenyezi Mungu mitume walipoweka mikono juu yao, akataka kuwapa fedha
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Simoni alingamua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Simoni alipoona, ya kuwa watu hupewa Roho, mitume wakiwabandikia mikono, akawaletea fedha,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Simoni alipoona kwamba wanafunzi wamepokea Roho Mutakatifu kwa njia ya kuwekewa mikono ya mitume, akaletea Petro na Yoane feza na kuwaambia:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta Simon alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekwa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha, akisema,