Acts 8:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo tubu kwa uovu huu wako na umwombe Mwenyezi Mungu. Yamkini aweza kukusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Badili moyo wako! Achana na mawazo haya maovu na umwombe Bwana. Yumkini atakusamehe!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo tubia huu uovu wako na umwombe Mungu, ili yamkini, aweze kusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo tubu kwa uovu huu wako na umwombe Mwenyezi Mungu. Yamkini aweza kukusamehe mawazo uliyo nayo moyoni mwako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili ikiwezekana, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sharti ujute na kuuacha huu uovu wako, ukimwomba Bwana, labda utapata kuondolewa mawazo ya moyo wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi ugeuke toka katika zambi zako na umwombe Bwana, labda atakusamehe kwa ajili ya mawazo ya namna hii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana illi, kama yumkini, usamebewe fikara lui ya moyo wako.