Acts 8:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara inayotoka Yerusalemu kuelekea Gaza ambayo ni jangwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jiandae na uende kusini katika barabara ya jangwani inayoteremka kutoka Yerusalemu kwenda Gaza.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Malaika wa Bwana akamwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza ambayo ni jangwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi malaika wa Mwenyezi Mungu akamwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza ambayo ni jangwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile iteremkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Malaika wa Bwana akamwambia Filipo akisema: Inuka, uende upande wa kusini, uifuate barabara itelemkayo toka Yerusalemu kwenda Gaza, ileile iliyokwisha kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Malaika wa Bwana akamwambia Filipo: “Ujitayarishe na uende upande wa kusini kupitia njia inayotelemuka toka Yerusalema kwenda katika muji Gaza, nayo ni njia watu wasiyozoea kupitia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka uende upande wa kusini hatta njia ile itelemkayo kutoka Yemsalemi kwenda Gaza; nayo ni jangwa.