Acts 8:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwanakondoo anapokatwa manyoya, yeye hakutoa sauti hata kidogo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko: “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni, kama mwana-kondoo anyamazavyo mbele yake yule amkataye manyoya, hivyo hakufungua kinywa chake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sehemu ya Maandiko aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kwa mchinjaji. Alikuwa kama mwana kondoo asivyopiga kelele anapokatwa manyoya yake. Hakusema kitu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwana kondoo anaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwanakondoo anapokatwa manyoya, yeye hakutoa sauti hata kidogo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la maandiko: “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni, kama mwana-kondoo anyamazavyo mbele yake yeye amkataye manyoya, hivyo hakukifungua kinywa chake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko: “Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni, kama mwana-kondoo anyamazavyo mbele yake yule amkataye manyoya, hivyo hakufungua kinywa chake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwanakondoo anapokatwa manyoya, yeye hakutoa sauti hata kidogo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo fungu la Maandiko, alilolisoma, lilikuwa hili: Kama kondoo alipelekwa kuchinjwa; kama mwana kondoo anavyomnyamazia mwenye kumkata manyoya, vivyo hivyo naye hakukifumbua kinywa chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na sehemu ya Maandiko aliyokuwa akisoma ni hii: “Alipelekwa kama kondoo kwenda kuchinjwa, kama mwana-kondoo anayenyamaza mbele ya mwenye kumukata manyoya. Yeye hakufungua kinywa chake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili: Alichukuliwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana kondoo asivyolia mbele yake amkatae manyoya, Vivyo hivyo yeve nae hafunui kinywa chake.