Acts 8:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake. Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake? Kwa maana maisha yake yaliondolewa kutoka duniani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alidhalilishwa, na kunyimwa haki zake zote. Maisha yake duniani yamekoma. Hivyo hakutakuwa simulizi yoyote kuhusu wazaliwa wake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake. Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake? Kwa maana maisha yake yameondolewa kutoka duniani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake. Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake? Kwa maana maisha yake yaliondolewa kutoka duniani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hivyo, alivyonyenyekea, alinyimwa uamuzi mnyofu; yuko nani atakayesimulia, ukoo wake ulivyokuwa? Kwani ameondolewa katika nchi yao walio hai, asikae nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alinyenyekezwa na kuhukumiwa bila haki. Hakuna mutu atakayeweza kueleza habari za kizazi chake, maana maisha yake yameondolewa katika dunia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakaeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika inchi.