Acts 8:34 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nini? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule towashi akamuuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Afisa akamwambia Filipo, “Tafadhali niambie, nabii anazungumza kuhusu nani? Anazungumza kuhusu yeye mwenyewe au mtu mwingine?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nini? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule towashi akamwuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena kwa habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule towashi akamuuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nini? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtunza mali akamwuliza Filipo akisema: Nakuomba, uniambie: Haya mfumbuaji anayasema ya nani? Anajisema mwenyewe au anamsema mwingine?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mukubwa akamwuliza Filipo: “Ninakusihi uniambie, nabii huyu anasema juu ya nani? Ni juu yake mwenyewe au juu ya mutu mwingine?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule tawashi akamjibu Filipo, Nakuomba, nabii huyu asema maneno haya kwa khabari ya nani; ni khabari zake mwenyewe an khabari za mtu mwingine?