Acts 8:39 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo towashi hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake mwenye furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao walipotoka kwenye maji, ghafula Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana akamchukua Filipo; afisa hakumwona Filipo tena. Afisa aliendelea na safari yake kurudi nyumbani, akiwa mwenye furaha sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa furaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo towashi hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake mwenye furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao walipopanda kutoka kwenye maji, ghafula Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao walipopanda kutoka kwenye maji, ghafula Roho wa Mwenyezi Mungu akamnyakua Filipo, naye towashi hakumwona tena, lakini akaenda zake akifurahi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo towashi hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake mwenye furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana alimpokonya Filipo, mtunza mali asimwone tena. Kisha akaishika njia yake na kufurahi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipotoka ndani ya maji, kwa rafla Roho wa Bwana akamutowesha Filipo, na yule mukubwa hakumwona tena, lakini akaongeza safari yake katika furaha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kiisha, walipotoka majini, Roho ya Bwana ikamnyakua Filipo, yule tawashi asimwone tena; maana alikwenda zake akifurahi: