Acts 8:40 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Injili mpaka alipofika Kaisarea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Filipo akajikuta Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote hadi akafika Kaisaria.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Filipo alionekana katika mji ulioitwa Azoto. Alikuwa akienda kwenye mji wa Kaisaria. Aliwahubiri watu Habari Njema katika miji yote wakati anasafiri kutoka Azoto kwenda Kaisaria.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Injili mpaka alipofika Kaisarea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Filipo akaonekana katika Azota, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hadi akafika Kaisaria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Injili mpaka alipofika Kaisarea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Filipo akaonekana Asdodi akiipiga hiyo mbiu njema katika miji yote, aliyoipita, hata akafika Kesaria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Filipo akajikuta amekwisha kuwa katika muji Azoto. Kisha akapita katika miji yote akihubiri Habari Njema, mpaka alipofika katika muji Kaisaria.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akakhubiri Injili katika miji yote, hatta akafika Kaisaria.