Acts 8:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza alizofanya, wakasikiliza kwa makini yale aliyosema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wa Samaria walimsikiliza Filipo na kuona miujiza aliyotenda. Wote walisikiliza kwa makini yale aliyosema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu walipomsikia Filipo na kuona ishara na miujiza aliyofanya, wakasikiliza kwa bidii yale aliyosema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mkutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
watu wengi wakashikamana na yale yaliyosemwa na Filipo, mioyo yao ikawa mmoja tu kwa hayo, waliyoyasikia na kuviona vielekezo, alivyovifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makundi ya watu waliposikia maneno yale Filipo aliyosema na kuona vitambulisho alivyoonyesha, wote walimusikiliza kwa nia moja na kwa uangalifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yote yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuiona miujiza aliyokuwa akiifanya.