Acts 9:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mfuasi yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
na kumwomba aandike barua kwenda kwenye masinagogi yaliyokuwa katika mji wa Dameski. Sauli alitaka kuhani mkuu ampe mamlaka ya kuwatafuta watu katika mji wa Dameski waliokuwa wafuasi wa Njia ya Bwana. Ikiwa angewapata waamini huko, wanaume au wanawake, angewakamata na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia ya Bwana, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye akamwomba Kuhani Mkuu ampe barua ya kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu ye yote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, wanaume kwa wanawake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akataka kwake barua za kwenda Damasko, aende nazo kwenye nyumba za kuombea za Wayuda, kwa maana alitaka kuwafunga na kuwapeleka Yerusalemu wo wote, atakaowaona wa njia hiyo, wakiwa waume au wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akataka ampe barua za kuenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kumwomba amwandikie barua za kumutambulisha katika nyumba za kuabudia za muji Damasiki. Katika barua hizo, Saulo alipewa ruhusa kwamba akiona watu wanaofuata Njia ya Bwana, ikiwa wanaume au wanawake, awafunge na kuwapeleka Yerusalema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.