Acts 9:27 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana Isa, jinsi Bwana alivyosema naye na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Isa huko Dameski.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Barnaba alimkubali Sauli, akamchukua na kumpeleka kwa mitume. Akawaeleza namna ambavyo Sauli alimwona Bwana akiwa njiani na namna ambavyo Bwana aliongea naye. Kisha akawaambia namna ambavyo Sauli amehubiri kwa ujasiri kuhusu Yesu katika mji wa Dameski.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila uoga kule Damasko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana, jinsi Bwana alivyosema naye na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana Isa, jinsi Bwana Isa alivyosema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Isa huko Dameski.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, Barnaba alipomchukua, akampeleka kwa mitume, akawasimulia, alivyomwona Bwana njiani, navyo alivyosema naye, tena alivyolitangaza Jina la Yesu huko Damasko waziwazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Barnaba akamutwaa na kumupeleka kwa mitume. Akawaelezea namna Saulo alivyomwona Bwana katika njia na jinsi Bwana alivyosema naye. Akawaelezea vilevile namna Saulo alihubiri kwa jina la Yesu pasipo woga katika Damasiki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu.