Acts 9:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo waumini katika Yudea yote, Galilaya na Samaria wakawa na wakati wa amani. Likatiwa nguvu; na kwa kuwezeshwa na Roho wa Mungu, idadi yao ikaongezeka, na wakaendelea kudumu katika kumcha Bwana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kanisa katika Uyahudi yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, vikundi hivi vya waamini vikawa na nguvu katika imani na kuonesha utii kwa ajili ya Bwana kwa namna walivyoishi. Hivyo kanisa kila mahali liliongezeka kwa idadi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo kanisa katika Uyahudi wote, Galilaya na Samaria likafurahia wakati wa amani. Likatiwa nguvu na likaendelea kudumu katika kumcha Bwana na kwa faraja ya Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo waumini katika Uyahudi wote, Galilaya na Samaria wakafurahia wakati wa amani. Wakatiwa nguvu, na kwa faraja ya Roho wa Mwenyezi Mungu, idadi yao ikazidi kuongezeka, na wakaendelea kudumu katika kumcha Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo kanisa likawa na amani popote katika Yudea, Galilaya, na Samaria. Lilijengwa na kukua katika kumcha Bwana, na kuongezeka likitiwa moyo na Roho Mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo wateule walitengamana pote katika Yudea na Galilea na Samaria, wakajijenga, wakaendeleana kwa kumcha Bwana, tena wakawa wengi wakitulizwa na Roho Mtakatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati ule, kanisa lilikuwa na amani katika Yudea yote, Galilaya na Samaria. Vilevile lilizidi kupata nguvu na kuendelea kumwogopa Bwana, nalo liliongezeka kwa musaada wa Roho Mutakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi makanisa wakapata raha katika Yahudi yote na Galilaya na Samaria, wakajengewa, wakiendelea katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.