Acts 9:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakaulaza katika chumba ghorofani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo akaugua, akafa, na wakauosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro alipokuwa Lida, Tabitha aliugua na kufa. Waliusafisha mwili wake na kuuweka chumbani ghorofani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakauzika katika chumba ghorofani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakaulaza katika chumba ghorofani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku zile akaugua, akafa; wakati walipokwisha kumwosha, wakamweka ghorofani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo ikawa kwamba aliugua, akafa. Watu wakauosha mwili wake, wakaulaza katika chumba ghorofani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, siku zile akaugua, akafa; kisha wakamwosha, wakamlaza katika chumba cha juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile akapata ugonjwa, naye akakufa. Walipokwisha kunawisha maiti yake, wakailalisha ndani ya chumba cha gorofi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa siku zile akaugua, akafa: hatta walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.