Acts 9:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akawatoa watu wote chumbani. Akapiga magoti na kuomba. Kisha akaugeukia mwili wa Tabitha na kusema, “Tabitha! Simama.” Akafumbua macho yake. Alipomwona Petro akaketi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akamgeukia yule maiti, akasema, “Tabitha, amka” Naye akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, inuka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Petero akawatoa wote, waje nje, akapiga magoti, akamwomba Mungu na kuugeukia ule mwili wake, akasema: Tabea, inuka! Ndipo, alipoyafumbua macho yake; alipomwona Petero akajiketisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro akawaamuru watu wote waende inje, akapiga magoti na kuomba. Kisha akaelekea ile maiti na kusema: “Tabita, simama!” Halafu Tabita akafungua macho, na wakati alipomwona Petro akaamuka na kuikaa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.