Amos 1:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Waliwawinda ndugu zao Waisraeli kwa mapanga, wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu. Hasira yao haikuwa na kikomo, waliiacha iwake daima.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, alikataa kuonesha huruma yoyote, kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararua-rarua daima, akaishika ghadhabu yake milele;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Waliwawinda ndugu zao Waisraeli kwa mapanga, wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu. Hasira yao haikuwa na kikomo, waliiacha iwake daima.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo BWANA asemalo: “Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, alikataa kuonyesha huruma yo yote, kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo bwana asemalo: “Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, alikataa kuonyesha huruma yoyote, kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararuararua daima, akaishika ghadhabu yake milele;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Edomu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Waliwawinda ndugu zao Waisraeli kwa mapanga, wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu. Hasira yao haikuwa na kikomo, waliiacha iwake daima.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Edomu matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa waliwakimbiza ndugu zao kwa panga, wakajizuia, wasiwahurumie, kwa kuwa waliendelea siku zote kuwanyafua kwa ukali, hawakomi kuwachafukia kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Edomu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, akatupilia mbali huruma zake zote; hasira yake ikararua-rarua daima, akaishika ghadhabu yake milele;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kwa sababu ya makosa matatu ya watu wa Edomu, hata kwa mane, sitageuza nia yangu. Wamewawinda wandugu zao Waisraeli kwa mapanga, wakaitupilia mbali huruma yao yote ya kindugu. Hasira yao haikuwa na mwisho, waliiacha iwake siku zote.