Amos 1:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Walichukua mateka watu kabila zima, wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Gaza, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima na kuwauza kwa Edomu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Walichukua mateka watu kabila zima, wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Kwa dhambi tatu za Gaza, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima na kuwauza kwa Edomu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Kwa dhambi tatu za Gaza, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima na kuwauza kwa Edomu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliliteka nyara kabila zima, wawatie katika mikono ya Edomu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Gaza wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Walichukua mateka watu kabila zima, wakawauza wawe watumwa kwa Waedomu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Gaza matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa waliwateka wote pia na kuwahamisha, wawapeleke utumwani kwa Waedomu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kwa sababu ya makosa matatu ya watu wa Gaza, hata kwa mane, sitageuza nia yangu. Wamekamata watu wengi na kuwapeleka kwa Waedomu.