Amos 1:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu, wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Tiro, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu, na kutokujali mapatano ya undugu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu, wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Kwa dhambi tatu za Tiro, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu, na kutokujali mapatano ya undugu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Kwa dhambi tatu za Tiro, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu, na kutokujali mapatano ya undugu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamelitia kabila zima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Tiro wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Walichukua mateka kabila zima hadi Edomu, wakaukiuka mkataba wa urafiki waliokuwa wamefanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Tiro matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa wote pia, waliowateka, waliwahamisha na kuwapeleka kwa Waedomu, hawakulikumbuka agano la Kindugu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kwa sababu ya makosa matatu ya watu wa Tiro, hata kwa mane, sitageuza nia yangu. Wamekamata watu wengi na kuwapeleka mpaka Edomu. Hawakutii mapatano ya urafiki waliokuwa wamefanya.