Amos 2:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomu kwa kuichoma moto mifupa yake ili kujitengenezea chokaa!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Moabu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu, ikawa kama chokaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomu kwa kuichoma moto mifupa yake ili kujitengenezea chokaa!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Kwa dhambi tatu za Moabu, hata kwa dhambi nne, sitazuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu, ikawa kama chokaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili ndilo asemalo bwana: “Kwa dhambi tatu za Moabu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu, ikawa kama chokaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomu kwa kuichoma moto mifupa yake ili kujitengenezea chokaa!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa ajili ya mapotovu ya Moabu matatu au manne sitayarudisha, yasiwapate, kwa kuwa mifupa ya mfalme wa Edomu waliichoma moto, hata ikawa chokaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa; Sef 2:8-11; 2 Fal 3:27
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema hivi: Kwa sababu ya makosa matatu ya watu wa Moabu, hata kwa mane, sitageuza nia yangu. Wamemukosea heshima marehemu mufalme wa Edomu kwa kuichoma mifupa yake kwa moto kwa kujitengenezea chokaa!