Amos 2:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwateua baadhi ya wana wenu wawe manabii, na baadhi ya vijana wenu wawe wanadhiri. Je, enyi Waisraeli, haya nisemayo si ya kweli? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu. Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwateua baadhi ya wana wenu wawe manabii, na baadhi ya vijana wenu wawe wanadhiri. Je, enyi Waisraeli, haya nisemayo si ya kweli? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu wa kiume. Je, hii si kweli, Enyi watu wa Israeli?” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu. Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwateua baadhi ya wana wenu wawe manabii, na baadhi ya vijana wenu wawe wanadhiri. Je, enyi Waisraeli, haya nisemayo si ya kweli? Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo miongoni mwa wana wenu nikainua wengine, wawe wafumbuaji, nao wengine nikawachagua katika vijana wenu, wajieue kuwa wangu. Au sivyo vilivyokuwa, ninyi wana wa Isiraeli? ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nilichagua manabii kati ya wana wenu, na wengine kati ya vijana wenu kuwa wanaziri. Enyi Waisraeli, haya ninayosema si ya kweli? –Ni ujumbe wa Yawe.–