Amos 2:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huwanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge, na maskini huwabagua wasipate haki zao. Mtu na baba yake hulala na mjakazi yuleyule, hivyo hulitia unajisi jina langu takatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini, kama vile juu ya mavumbi ya nchi, na kukataa haki kwa waliodhulumiwa. Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja, kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nao hutwetea mavumbi yaliyo juu ya vichwa vya maskini, na kuipotosha njia ya mwenye upole; na mtu na baba yake humwendea mwanamke mmoja, hata kulitia unajisi jina langu takatifu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huwanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge, na maskini huwabagua wasipate haki zao. Mtu na baba yake hulala na mjakazi yuleyule, hivyo hulitia unajisi jina langu takatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini kama vile juu ya mavumbi ya nchi na kukataa haki kwa walioonewa. Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja, kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini, kama vile juu ya mavumbi ya nchi, na kukataa haki kwa walioonewa. Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja, kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nao hukanyaga vichwa vya maskini katika mavumbi ya nchi na kuwasukuma walioteseka kwenye njia yao; na mtu na baba yake wanamwendea mwanamke mmoja, na kulitia unajisi jina langu takatifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huwanyanyasa na kuwakandamiza wanyonge, na maskini huwabagua wasipate haki zao. Mtu na baba yake hulala na mjakazi yuleyule, hivyo hulitia unajisi jina langu takatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanatunukia na kutwetatweta, mavumbi ya nchi yawe vichwani juu yao wakiwa, nazo njia za wanyonge huzipotoa. Mtu na baba yake pamoja humwendea mwanamke mgoni, Jina langu takatifu walipatie uchafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nao hutwetea mavumbi yaliyo juu ya vichwa vya maskini, na kuipotosha njia ya mwenye upole; na mtu na baba yake humwendea mwanamke mmoja, hata kulitia unajisi jina langu takatifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanagandamiza wazaifu, na kuwabagua wamasikini wasipate haki zao. Mutoto na baba yake wanalala na binti mujakazi mumoja, hivyo wanalichafua jina langu takatifu.